Mkuu wa chuo Ndg. Augustine J. Sahili akiwa sambamba na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Ualimu Morogoro wakiwapokea wageni kutoka nchi za umoja wa Ulaya.
Mkuu wa Chuo Ndg. Augustine J. Sahili alizungumza kwa kuanza na historia ya chuo tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa. Kwa sasa Chuo cha Ualimu Morogoro kina wanachuo 1024 wa kike kwa wa kiume na wanafunzi wote hawa hupata huduma za malazi na chakula ndani ya chuo.
Mkuu wa chuo aliendelea kuongea na wageni (mabalozi) kuhusu utumiaji wa nishati safi kwa ajili ya kupikia. Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliweka malengo kuhama kutoka matumizi ya kuni katika kupikia na kutumia gesi safi pamoja na kuni poa.
Uongozi wa Chuo cha Ualimu Morogoro kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilifanya maamuzi ya kuhama kwenda matumizi ya gesi safi na kuni poa. Mchakato wa gharama ulifanyika na matumizi rasmi ya gesi safi ulianza mwanzoni mwa mwaka 2019 sambamba na kuni poa Julai ya 2023.
Ununuzi huu wa vifaa na marekebisho ya majiko pamoja na uwezweshaji wa wapishi juu ya matumizi ya gesi safi na kuni poa ulisimamiwa na kufanywa na chuo. Kampuni ya gesi ya Taifa imekua ni msambazaji wa gesi hii safi kwa matumizi ya kupikia lakini pia kampuni hii imekua ikifanya marekebisho ya mfumo panapokua na tatizo.
Pamoja na hayo makadirio ya matumizi tani 2 ya gesi safi hutumika kwa miezi miwili na tani 10 ya kuni poa kwa miezi saba.
Kwa kumalizia Mkuu wa chuo alishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na washirika kwa kuwezesha zoezi hili la gesi safi na kuni poa. Pia aliainisha faida za matumizi ya gesi safi na kuni poa; ikiwa ni pamoja na:
Kupunguza uharibufu wa mazingira.
Imekua rahisi sasa, milo ya wanachuo hupikwa na kutengwa kwa wakati.
Kuni poa ni bei rahisi tofauti na kuni zilizokua zinatumika mwanzo.
Haikugharimu gharama kubwa kufanya marekebisho ya majiko kwa ajili ya kuni poa. Majiko yale yale ya mwanzo yanatumika.
Wageni walipata nafasi ya kwenda kuona mifumo ya gesi pamoja na matumizi yake jikoni.