Chuo cha Ualimu Morogoro kinashuhudia kuongezeka kwa ubunifu na ujasiriamali miongoni mwa wanachuo wake, huku ikikuza vipaji na uwezo wa vijana hawa. Klabu hii, yenye wanachama 61, imekuwa kitovu cha kujifunza na kupeana uzoefu katika nyanja mbalimbali za ujasiriamali. Klabu hii imejitolea kuwajengea wanafunzi ujuzi na uwezo wa kujitegemea kwa kuwashirikisha katika miradi mbalimbali ya ujasiliamali. Vitengo sita vikuu vya klabu hii, ambavyo ni utengenezaji wa sabuni, uandaaji wa video na picha, uchoraji, mapishi, kilimo na ufugaji, na mapambo, vimewapa wanafunzi fursa ya kuchunguza na kukuza vipaji vyao katika maeneo haya.
Kupitia vitengo hivi, wanafunzi wanapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo, kuunda bidhaa na huduma mbalimbali, na kupata uzoefu wa kuendesha biashara ndogo ndogo. Kwa mfano, wanafunzi wanaojishughulisha na utengenezaji wa sabuni wanajifunza kuhusu viambato vya asili, mchakato wa utengenezaji, na uuzaji wa bidhaa zao.
Kwa ujumla, klabu ya ujasiliamali ya Chuo cha Ualimu Morogoro imekuwa jukwaa muhimu kwa kukuza vipaji na uwezo wa wanafunzi. Kwa kuwajengea ujuzi wa ujasiliamali, klabu hii inachangia katika kuandaa vijana wenye uwezo wa kujitegemea na kuchangia katika maendeleo ya jamii.