Siku ya wafanyakazi duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 1 Mei. Chuo cha Ualimu Morogoro ni miongoni mwa taasisi ambazo zilifanikiwa kufanya maadhimisho hayo kwa kukusanyika kwa pamoja.

Kamati ya Ustawi iliratibu sherehe hii kwa kuwakutanisha Wafanyakazi wa Chuo cha Ualimu Morogoro na kupata chakula cha mchana kwa pamoja.

Katika sherehe hiyo wafanyakazi ambao ni wanajamii wa chuo Cha Ualimu Morogoro walibadilishana mawazo katika maswala mbalimbali yahusuyo ustawi wao. Pia walipongeza kamati kwa kuratibu masuala mbalimbali ya kijamii na walipendekeza mikutano hiyo ifanyike mara kwa mara kwa maana inawafanya kuondoa uchovu wa kazi na kuhusiana zaidi na hivyo kujenga umoja na mshikamano kati yao.

Matukio katika picha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *