Chuo cha Ualimu Morogoro kilifurahia tukio la kipekee la Mahafali ya 53, ambapo jumla ya wahitimu 354 walitambuliwa kwa mafanikio yao makubwa. Sherehe hizi za kipekee zilifanyika chini ya uongozi thabiti wa Mkuu wa Chuo Augustine Sahili, ambaye ameendelea kuongoza chuo hicho kuelekea mafanikio makubwa.
Mgeni rasmi katika mahafali haya alikuwa Ndugu Joel Mwageni, Meneja wa CRDB Morogoro, ambaye alitoa hotuba yenye busara na kutia moyo wahitimu hawa katika safari yao ya baadaye. Ndugu Joel Mwageni aliwapongeza wahitimu kwa juhudi zao na kuwahimiza kuwa ujuzi walioupata ukanufaishe Taifa, lakini pia kujijengea Utama duni wa kujiwekea akiba na kuwakumbuka wazazi mara baada ya kupata mafanikio. Alihitimisha hotuba yake kwa kuzipokea changamoto zote zilizotolewa kupitia risala na kuahidi kuzifanyia kazi.
Wahitimu hawa 354 wanastahili pongezi kwa kujituma na kufanya vizuri katika masomo yao. Wameonyesha uwezo wa juu na bidii katika kipindi chote cha masomo yao, na sasa wanajiandaa kuingia katika ulimwengu wa kazi wakiwa tayari kukabiliana na changamoto zozote zinazowakabili.
Mahafali ya 53 ya Chuo cha Ualimu Morogoro yalikuwa ni tukio la kipekee linalothibitisha azma ya chuo hicho katika kuandaa wataalamu bora na wenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Tunawatakia wahitimu wote mafanikio makubwa katika safari yao ya baadaye na tunatarajia kuona mchango wao katika maendeleo ya taifa letu. Hongera sana kwa wahitimu wote!
2 thoughts on “Mahafali ya 53 ya Chuo cha Ualimu Morogoro: Kuenzi Mafanikio ya Wahitimu”
Hakika Chuo Cha Ualimu Morogoro ni mahala salama na sahihi kabisa kwa kupika nguvu kazi ya Taifa lijalo katika nyanja za taaluma, maadili, usafi na mazingira ya jamii zetu.
#People_Deserve_To_Know👌
Hakika Chuo Cha Ualimu Morogoro ni mahala salama na sahihi kabisa kwa kupika nguvu kazi ya Taifa lijalo katika nyanja za taaluma, maadili, usafi na mazingira ya jamii zetu.
#People_Deserve_To_Know👌
HABARI mkuu nlkuwa nauliza udahiri kwa mwaka wa MASOMO 2024-2025 yanaanza lini?