Mrejesho wa tathmini ya shughuli za TESP

0

Mrejesho huu uliandaliwa na kuwasilishwa na Mkuu wa Chuo Augustine J. Sahili pamoja na Mkufunzi Moshi H. Ngogomela, Mratibu wa Dawati la Jinsia na Ujumishi Chuo cha Ualimu Morogoro.

Katika uwasilishaji huo wafanyakazi wote walipata wasaa wa kushirikishwa katika maeneo mbalimbali ambayo TESP imetekeleza katika vyuo vya ualimu.

Taarifa hii inahusisha toleo la tarehe 04.04.2024 (bofya hapa kutazama) pamoja na makala fupi (bofya hapa kutazama).

Washiriki pia walipata fursa ya kuchangia mikakati mbalimbali ambayo itawezesha Chuo cha Ualimu Morogoro kuendeleza shughuli zilizotekelezwa na TESP.

Miongoni mwa mikakati hiyo ni:
  1. Uwepo wa chumba cha kubadilishia. Kuwawezesha wanachuo kupata vifaa vyote vya msingi pindi inapohitajika (ikiwemo taulo za kike, mafuta, sabuni, vitana n.k)
  2. Maboresho ya miongozo katika vyuo vya ualimu. Maboresho haya yatasaidia sheria, kanuni na taratibu zilizopo vyuo vya ualimu kuendana sawa na miongozo inayotoka wizarani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *