Shirika la Lyra in Africa yakabidhi komputa za msaada katika Chuo Cha Ualimu Morogoro. Mahusiano na Ushirikiano mzuri baina ya Mashirika binafsi, Serikali na Chuo Cha Ualimu Morogoro yamekuwa chachu ya mafanikio Chuoni.
Mkurugenzi wa Lyra in Afrika katika makabidhiano hayo ya Komputa alisistiza kuwa ulimwengu unakuwa kwa kasi hivyo ni muhimu kuandaa walimu wanaoendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia. Aidha Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Morogoro alitoa shukrani za dhati kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wafadhili mbalimbali katika kutimiza adhima ya Serikali ya kuleta maendeleo katika Elimu.
Kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugezi Msaidizi Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule sehemu ya Vyuo vya Ualimu ndugu Mathias Mvula alipongeza jitihada za Chuo katika kuimarisha mahusiano bora. Katika hotuba yake aliwasilisha salamu za pongezi kutoka Wizarani na kuomba Lyra kuendelea kusaidia Vyuo vya Ualimu katika maeneo mengine tofauti kama vile ukarabati wa miundombinu kama Mabweni. Mkurugenzi ndugu Mathias Mvula alikamilisha hotuba yake fupi kwa kusistiza kuwa Komputa zilizoletwa zitumike katika malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuzisaidia shule za jirani na Chuo.