Mafunzo kabilishi kwa wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro yaliyoanza tarehe 16 – 17/04/2024 na kuwajengea wakufunzi uelewa mpana kuhusu mtaala ulioboreshwa. Mafunzo yalihusisha Uchambuzi wa mtaala na vifaa vyake, Matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji, Mbinu za ufundishaji na ujifunzaji, uchopekaji wa masuala mtambuka na upimaji na tathmini.
Mafunzo haya yaliyohusisha wakufunzi 97 kutoka Chuo cha Ualimu Morogoro na yaliwezeshwa na wataalam watatu Dr. Wadrine Maro, Ndugu Merina Yohana na Ndugu Radhia Shemlugu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania. Mafunzo haya yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa Chuo – Morogoro Ndugu Augustine Sahili na kufungwa na Makamu Mkuu wa Chuo Ndugu Gwambazi Magubike.